Thursday, June 1, 2017

UEFA Yapitisha Sheria Mpya Kuelekea Fainali Juve & Real Madrid

Kwa lengo la kulinda utimamu wa wachezaji shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA imepitisha sheria mpya ambayo itaziwezesha timu kufanya mabadiliko (substitution) mara nne badala ya mara tatu ambayo ilikuwepo awali endapo tu mechi itaenda hatua ya dakika 30 za nyongeza.


Kwa sasa timu inaruhusiwa kufanya mabadiliko (Sub) kwa wachezaji watatu tu bila kujali ni kwa muda gani mechi itachezwa kwa maana iwe ni dakika 90 za kawaida au dakika 120, lakini kwa sheria hii mpya ni kwamba makocha hawatakuwa tena na hofu ya kufanya mabadiliko wakihofia kumaliza mapema idadi ya wachezaji inayoruhusiwa ikiwa matokeo yatakuwa ni ya sare kwa muda wa kawaida wa dakika tisini.

Sheria hii itaanza kufanya kazi katika mchezo wa fainali kati ya Juventus dhidi ya Real Madrid itakayopigwa jijini Cardiff huko nchini Wales Juni 2 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment