Tuesday, March 28, 2017

Tambwe wa Yanga Morris wa Azam fit kwa pambanano April 1


Wakati zikiwa zimebakia siku 4  jumamosi April 1, kwa mchezo unaosubiriwa kwa hamu kati ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania timu ya Yanga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati timu ya Azam  habari njema ni kupona kwa wachezaji muhimu wa timu hizo.

Kwa upande wa Azam ukuta wake uliondokewa na beki wake kisiki Aggrey Morris, Morris alipata majeraha hayo wakati Azam FC ikiichapa Mbabane Swallows bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo katikati ya wiki iliyopita alianza programu ya mazoezi ya ‘gym’ kabla ya leo kuhamia uwanjani.

Kwa upande mwingine kilabu ya Yanga ambayo ilipata wakati mgumu wa kucheza na Zanaco bila kuwa na washambuliaji wa kati, leo mchezaji tegemeo kwa ufungaji Amis Tambwe ameanza rasmi kujifua uwanjani baada ya kupona majeraha yake.

Tambwe na Ngoma wamekuwa majeruhi toka kombe la Mapinduzi . . Kwa nyakati tofauti wamejaribu kurudi uwanjani hata hivyo majeraha hayo yaliwarudisha nje tena! Baada ya mazoezi ya Gym , jana Tambwe aliungana na wenzie mazoezi ya uwanjani. Hali ni tofauti kwa Ngoma ambaye bado ni mgonjwa

0 comments:

Post a Comment