Wednesday, September 14, 2016

AZAM VS SIMBA KUPIGWA DIMBA LA UHURU

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na Simba ya Dar es Salaam, utafanyika Jumamosi Septemba 17, 2016 kama ilivyopangwa awali.

Ila mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam badala ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu za kuipa nafasi timu ya taifa ya vijana ya mpira wa miguu ya Congo Brazzaville ambayo itakuwa nchini kwa ajili ya mchezo wa ushindani dhidi ya wenyeji – Serengeti Boys ambayo ni timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Timu hizo zinakutana kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo. Mchezo huo utafanyika Septemba 18, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam hivyo kutokana na kanuni za mashindano, siku moja kabla mgeni anapata nafasi ya kufanya mazoezi.

Serengeti Boys ambayo ilipiga kambi Shelisheli kujiandaa na mchezo huo ambako imejipanga vyema kuiondoa Congo Brazzaville katika michezo miwili inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali ukianzia huo wa Septemba 18, 2016 kabla ya kurudiana jijini Brazzaville hapo  Septemba 30 au Oktoba 1 au Oktoba 2, mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa (CEO) Azam FC, Saad Kawemba kwa mujibu wa kanuni ya 6 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kipengele cha 5 na 6, ameridhia mchezo huo kufanyika Uwanja wa Uhuru hapo Septemba 17, 2016 na kufuta upotoshwaji unaofanyika kwenye mitandao ya kijamiii.

Kawemba alizungumza hayo, mara baada ya kupokea Ngao ya Hisani halisi mara baada ya tuzo hiyo kufika jijini Dar es Salaam ikitokea China pamoja na vifaa vingine. Itakumbukwa kwamba awali Agosti 17, 2016 mara baada ya kuishinda Young Africans kwa mikwaju ya penalti, Azam walipewa Ngao ya mfano.
CHANZO: TFF
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

Related Posts:

  • SIMBA YAIFUATA MAJIMAJI SONGEA Kikosi cha Simba kimesafiri alfajiri ya leo kuelekea Songea tayari kwa mchezo wake dhidi ya Majimaji FC. Simba itaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa awali dhidi ya Mwadui FC, hivyo kuh… Read More
  • HASSAN RAMADHANI KESSY AMWAGA WINO YANGA Beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Ramadhani Kessy (katikati) akitia dole gumba kwenye fomu za Mkataba wa Yanga, Kessy amesaini miaka miwili kuitumikia Yanga kuanzia mwezi ujao. Zoezi hilo lilifanyika juzi usiku mjini Dar… Read More
  • HIKI NDO KIKOSI CHA SERENGETI BOYS Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi amewataka wachezaji wa timu ya soka ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama jina la Serengeti Boys kwenda kucheza soka la ushi… Read More
  • TFF YAZIKUMBUSHA TENA KLABU ZA LIGI KUU 2016/17 Kwa mara nyingine, Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezikumbusha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kuwa mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza tangu Mei 5, 2016. Bodi ya Ligi… Read More
  • TAZAMA MASHABIKI WA SIMBA WALIVYOLIANZISHA MSIMBAZI Kufuatia matokeo mabaya yanayoikumba klabu ya Simba katika mechi zao za hivi karibuni, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wameshindwa kuvumilia na kuamua kujikusanya katika makao makuu ya klabu hiyo kwa kile wanachodai … Read More

0 comments:

Post a Comment