Aliyekuwa mjumbe kamati ya utendaji Simba Said Pamba amefariki dunia Jana Jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo jumatatu saa 5 Asubuhi.
Pamba alikuwa mjumbe katika kamati hiyo chini ya uongozi wa Ismail Aden Rage, Pamba amekutwa na umauti huo katika Hospitali ya Mbezi alikokuwa anapata matibabu.
"Msiba upo Manzese Darajani kwa dada yake, tumepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa, Pamba alikuwa ni mtu ambaye alisikiliza ushauri na mtendaji mzuri mwenye misimamo yake, hivyo tumepoteza mtu muhimu katika soka letu" alisema Nkwabi rafiki wa karibu wa marehemu alipozungumza na Mwanaspoti.
Pamba ameacha Mke na watoto watatu.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMEEN
0 comments:
Post a Comment