Mabingwa
wa soka Tanzania, Yanga watakuwa kibaruani Jumamosi kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam kuwavaa Al Ahly kutoka Misri katika mechi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tayari wachuuzi, wameanza kuuza jezi za Al Ahly katika anga mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
Lakini
hilo halijamtisha Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga,
Jerry Muro ambaye ameamua kuwaalika Simba na Azam FC waungane Jumamosi.
Muro amesema anaamini huu ni wakati wa uzalendo, wakati wa Utanzania na si upinzani wa Ligi Kuu Bara.
“Kweli nataka waje tuungane, kwani umesikia hata Simba nikiwatania? Sifanyi hivyo kwa kuwa ni kipindi cha kuungana.
“Hata Azam FC waje Jumamosi, mimi pia niende kuwashangilia Jumapili. Mambo ya utani yatarudi baada ya hii michuano ya kimataifa.
“Mfano
Simba nao wakifuzu siku moja, nitaungana nao kuwashangilia. Sidhani
kama ni sahihi kuwashangilia wageni wakati sisi ni Watanzania,” alisema
Muro.
0 comments:
Post a Comment