Wednesday, April 13, 2016

Kwa Mchezo Huu Wakimataifa Wajitazame Upya.

Ligi ya vodacom imeendelea tena Leo katika viwanja viwili.
Mjini Morogoro Mtiwa Sugar waliikalibisha Azam Fc wakati Yanga ikicheza na Mwadui Fc ya Mjini Shinyanga katika uwanja wa taifa.

Azam Fc imecheza katika mazingira magumu ya uwanja wa Mtibwa uliokuwa umejaa Maji lakini walifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Mtibwa Sugar, goli lililofungwa na John Bocco dakika ya 61' kwa mkwaju wa penati kufuatia rafu aliyochezewa mchezaji wa Azam katika eneo la hatari.

Katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Yanga imeibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya Mwadui Fc, Yanga imeonyesha kiwango kibovu sana ikizingatiwa kuwa inashiriki mashindano ya klabu bingwa na wanamchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly April 19. Yanga wanatakiwa kuimarisha kikosi chao ili waweze kuleta ushindani mkubwa pale watakapoenda kucheza na Al Ahly.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva Dakika ya 13 na Harouna Niyonzima dakika ya 86.
Kwa matokeo hayo Yanga inafikisha pointi 56 ikiwa imeshacheza michezo 23 katika nafasi ya pili. Azam Fc nao kwa matokeo ya Leo wanafikisha pointi 55 katika nafasi ya tatu ikiwa imekwishacheza mechi 24 sawa na simba anaeshika nafasi ya kwanza kwa pointi 57.

0 comments:

Post a Comment