Wednesday, April 13, 2016

"Wadhihirishieni kuwa Barcelona Ndio Klabu Bora Zaidi Ulaya." Enrique


Kocha wa Barcelona Louis Enrique amewaomba vijana wake waudhihirishie ulimwengu leo kuwa timu hiyo ndio bora zaidi kwa sasa Barani ulaya na Dunia kwa ujumla.

Barcelona ambayo leo inacheza na Atletico Madrid katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Barani Ulaya iliibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja katika mchezo wa kwanza uliocheza katika dimba la Camp Nou. Leo wanaingia uwanjani wakiwa na faida ya magoli mawili waliyoyapata wakiwa nyumbani lakini goli moja la Fernando Torres walilolipata Atletico wakiwa ugenini ni mtaji mkubwa pia kwao.


Enrique aliyasema hayo kuelekea mchezo wao wa leo katika uwanja wa Calderon akisema “ Tuna  nafasi ndogo lakini bado mchezo uko wazi kwa atakaecheza vizuri kushinda, tutapambana tuweze kushinda na timu yangu imejiandaa kuyakabili mazingira yote yanayotusubiri katika mchezo wa leo. Kama kuna timu ambayo inaweza kuendana na mazingira ya uwanja wa Vicente Calderon basi timu hiyo ni Barca. Tunajua kwamba tunatakiwa kucheza mchezo mzuri ili tuweze kushinda”

Kichapo walichokipata wazee hao wa Camp Nou wikiendi iliyopita kutoka kwa Real Sociedad kimeifanya Barcelona kucheza mechi 3 bila kushinda huku wakiacha nafasi wazi kwa Atletico na Real Madrid kufufua matumaini yao ya kufukuzia ubingwa wa La Liga.

0 comments:

Post a Comment