Wednesday, May 4, 2016

HONGERENI AZAM FC KWA HILI MNALOLIFANYA


Azam FC inawakaribisha vijana wote Tanzania mwenye  umri chini ya  miaka 20 yani (U-20), nenda kajaribu bahati yako ya kufanya majaribio na kujiunga na 'Azam FC Academy' Jumamosi hii Mei 7 ndani ya makao makuu ya Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Majaribio hayo yataanza rasmi saa 2.00 asubuhi, hivyo Benchi la Ufundi la timu ya vijana ya Azam FC chini ya Tom Legg na Idd Cheche, linawaomba vijana muzingatie muda kwa kufika mapema popote ulipo nchini.

Azam FC  imekuwa na utaratibu wa kuendesha zoezi la majaribio kwa vijana wa umri huo kila Jumamosi ya kwanza ya ya kila mwezi, lengo likiwa ni kuvumbua vipaji na kuwapa nafasi vijana kuonyesha uwezo wao ili hatimaye baadaye wapate nafasi ya kujiunga na Academy ya Azam FC.

0 comments:

Post a Comment