Wednesday, May 4, 2016

TSH. 15,000/- YA LEIGH HERBERT SHABIKI WA LEICESTER CITY YAMFANYA KUWA MILIONEA


Anaitwa Leigh Herbert,Ana miaka 39, Ni Fundi seremala Na Ni shabiki wa Leicester City, Mwanzoni kwa msimu wa ligi kuu England mwaka Jana mwezi wa 8, akiwa amelewa pombe alitabiri kuwa Leicester City watatwaa ubingwa wa ligi kuu, alichukua paundi 5, ambazo Ni sawa Na Sh. Elf 15880/- za Tanzania akacheza kamali hiyo. Juzi Usiku Leicester  City wamekuwa mabingwa wapya wa EPL msimu huu, hivyo bwana Leigh kushinda kamali hiyo. kutokana Na kupatia Utabiri huo atapewa paundi elf 20,600, sawa Na Sh. Milioni  Sitini na Tano, Laki Nne na Elf Tisa mia Tisa Arobaini (65,409,940/-)

Leigh amesema fedha hizo atachukua baadhi atafanyia sherehe na zingine atazitumia kuboresha nyumba yake.

0 comments:

Post a Comment