Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Hamisi Tambwe ndiye anaongoza katika chati ya ufungaji bora ligi Kuu Tanzania bara Msimu huu wa 2015/2016. Tambwe ambae jana alifunga goli katika mechi dhidi ya Stand United, alifikisha jumla magoli 20, akiifikia rekodi iliyokawekwa na Abdalah Juma mwaka 2006 ya kufikisha idadi hiyo ya magoli katika msimu mmoja akiichezea Mtibwa Sugar.
Wachezaji wengine ambao wapo katika chati hiyo ya Ufungaji bora ni:
1: Hamisi Kiiza 19
2: Donald Dombo Ngoma 16
3: Elias Maguri 11
4: Kipre Herman Tchetche 10
0 comments:
Post a Comment