Saturday, April 9, 2016

Yanga Na Azam Kuipa TFF Mamilioni Ya Pesa


Achana na klabu zenyewe kuneemeka, Azam FC na Yanga zikifuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho basi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litapata fedha kutokana ushiriki wa timu hizo.

Yanga ipo katika Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ikitolewa na Al Ahly itakwenda kwenye Kombe la Shirikisho ambako inaweza kufuzu hatua ya makundi sawa na Azam ambayo tayari ipo katika michuano hiyo.
Azam yenyewe inatakiwa kwanza kuitoa Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora, halafu icheze tena mtoano na timu kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika ndipo ifuzu hatua ya makundi.

Kuna uwezekano mkubwa Azam na Yanga ama kukutana katika makundi Kombe la Shirikisho au zenyewe kucheza mtoano kuwania kufuzu hatua hiyo.
Kama zote zikifuzu hatua za makundi basi kila timu haikosi dola 150,000 sawa na Sh milioni 321 ambayo ni zawadi ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa timu inayoshika mkia miongoni mwa timu nne
.
Utaratibu wa Caf ni kutoa fedha pia kwa shirikisho au chama cha soka ambako timu inatokea, hivyo kwa anayeshika nafasi ya nne chama chake cha soka kitapata dola 15,000 sawa na Sh milioni 32.


Ikiwa Azam na Yanga zikifuzu, TFF itapata Sh milioni 64, timu ikishika nafasi ya tatu itapata dola 239,000 sawa na Sh milioni 511, hapo TFF itapata dola 20,000 sawa na Sh milioni 42. Kucheza nusu fainali ni sawa na aliyeshika nafasi ya tatu.

Bingwa atapata dola 625,000 sawa na Sh bilioni 1.3 na TFF hapo itapata dola 35,000 sawa na Sh milioni 74. Mshindi wa pili atapata dola 432,000 sawa na Sh milioni 924 na TFF itapata dola 30,000 sawa na Sh milioni 64.

Related Posts:

  • SIMBA YAITOLEA NJE YANGAKlabu ya Simba imekanusha taarifa zilizotolewa na Ofisa habari wa Yanga Jerry Muro kuwa waliandikiwa barua ya kutaka kutoa ruhusa ya Kessy. Kessy amesajiliwa na Yanga akitokea Simba na amezuiwa kucheza kutokana na mkataba … Read More
  • ONYO KALI NA MUHIMU KWA YANGA KUELEKEA MECHI YAO LEOMwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage amesema wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga hawana leseni za kuichezea timu hiyo katika mchezo wa leo. Rage amesema Sheria ya Usajili ya michuano ya Kombe la shirikisho namba … Read More
  • VIDEO: TAZAMA HALI ILIVYO UWANJA WA TAIFA ASUBUHI HII YANGA VS TP MAZEMBE Mashabiki wakiwa wamefurika nje ya uwanja wa taifa wakisubiri mechi kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe leo jioni Hawa tayari wameshaingia Ndani ya Uwanja  Like Ukurasa Wa Soka24 Face… Read More
  • HATIMAYE TAMBWE AFUNGUKA UJIO WA CHIRWA YANGAMshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema kucheza timu kubwa kama Yanga kunahitaji ujasiri kutokana na usajili unaofanywa kila wakati. Ujio wa mshambuliaji mpya kwenye kikosi cha Yanga, Mzambia Obrey Chirwa, unaonekana … Read More
  • HII NDO HALI ILIYOPO UWANJA WA TAIFA WATU WAMEFURIKA Kuelekea Mchezo kati ya Yanga na TP Mazembe Leo Jioni Hivi Ndivyo Mashabiki Walivyofurika Uwanja Wa Taifa Mapema Leo Kusubiri Mchezo Huo. KILA LA KHERI YOUNG AFRICA Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa … Read More

0 comments:

Post a Comment