Jina la Cristiano Ronaldo kwa sasa tayari limekwisha andikwa katika kila kitabu cha rekodi za mpira wa miguu Ulimwenguni.
Amefunga magoli mengi katika ligi kubwa Barani Ulaya kuliko mchezaji yeyote. Ni mchezaji wa kwanza na hakuna mwingine, kufikisha magoli 100 katika mashindao ya klabu bingwa barani Ulaya.
Ana rekodi pia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuingia katika kitabu cha rekodi za Dunia (The Guinness World Record) kwa kuwa mchezaji mwenye LIKES nyingi zaidi katika mtandao wa Facebook.
Hata hivyo, kwa magoli mawili aliyoyapachika katika mchezo wa fainali jana dhidi ya Juventus, Mtaliano huyo ameziweka rekodi mpya kabisa katika historia yake ya soka.
Hapa Chini ni baadhi tu ya Rekodi ambazo kupitia mchezo wa fainali wa jana Ronaldo ameziweka.
1. Amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali 3 za UEFA Champions League
Baada ya kufunga goli katika fainali ya mwaka 2008 akiwa na klabu ya Manchester United, na mkwaju aliopachika katika fainali ya mwaka jana, Ronaldo tena amefanikiwa kufunga goli la kwanza na la tatu katika fainali ya jana dhidi ya Juve.
Kabla Hujabisha: Messi amefunga katika fainali mbili tu, (2009 na 2011)
2. Amemfunika Messi kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Klabu Bingwa Barani Ulaya msimu huu 2016/17 baada ya kuachwa nyuma kwa tofauti ya magoli 7 katik yake na Messi.
Kabla ya mechi kati ya Bayern na Madrid iliyopigwa Ujerumani April 12 mwaka huu, Ronaldo alikuwa amefunga magoli 2 tu huku Messi akiwa amekwishapachika magoli 10, hivyo kufanya tofauti kati ya Ronaldo na Messi kuwa ni magoli 7, lakini Ronaldo alifunga magoli 2 katika mechi ya kwanza dhidi ya Bayern kisha akapiga hat-trik katika mchezo wa marudiano na kumfanya afikishe magoli 7, na kupunguza gap la magoli kati yake na Mesi kutoka 7 hadi kuwa 3. Mesi aliongeza goli katika mchezo dhidi ya PSG na kufikisha magoli 11, lakini Katika mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid, CR7 alipiga hat-trik na kumfanya afikishe idadi ya magoli 10, goli moja nyuma ya Mesi.
Hata hivyo kabla ya mechi ya fainali ya jana Ronaldo alikuwa amekwisha pachika magoli 10 akizidiwa goli 1 na Messi ambaye klabu yake iliondolewa katika hatua ya Nusu fainali na Juventus.
CR7 jana alifanikiwa kuweka kambani magoli mawili na kumfanya afikishe idadi ya magoli 12 goli moja zaidi mbele ya Messi, Hivyo Ubingwa jana ulifurahiwa mara mbili na Ronaldo, kwanza alikuwa anafurahia kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na klabu yoyote tangu kuanzishwa kwa klabu bingwa Ulaya, Pili kuibuka mfungaji bora katika michuano hiyo huku akimpiku mpizani wake wa karibu Lionel Messi.
3. Amekuwa Mfungaji Bora wa UEFA Champions League Mara Nyingi zaid kuliko mchezaji mwingine yoyote.
Ronaldo na Messi kabla ya mechi ya fainali ya jana wote walikuwa sawa katika kutwaa zawadi ya ufungaji bora klabu Bingwa ulaya, wote wakichukua tuzo hiyo mara tano. Lakini baada ya kuibuka tena mfungaji bora msimu huu uliomalizika kwa fainali ya jana CR7 anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mfungaji bora mara 6.
4. Amefikisha magoli 600 katika maisha yake ya soka.
5. Amefikisha magoli 500 akiwa na klabu ya Real Madrid
Goli lake la kwanza limeifanya Real Madrid kuwa timu ya kwanza kufikisha magoli 500 katika michunao ya UEFA Champions.
6. Amekuwa Mchezaji wa 20 katika historia ya soka kushinda makombe 4 au zaidi ya Ulaya.
Ushindi wa jana Cardiff umempa taji la 3 Ronaldo katika makombe ya Ulaya akiwa na Madrid, ukiongezea na Moja aliloshinda mwaka 2008 akiwa na Manchester United. Ni wachezaji 19 tu ambao wameweza kufanikiwa kufanya hivyo na kati ya hao, wachezaji 11 wanatoka katika klabu ya Real Madrid kuanzia miaka ya 1950s.
7. Amefikia rekodi ya Raul ya kucheza mechi 144 za UEFA Champions League akiwa katika nafasi ya 4 katika list ya wachezaji wa muda wote waliocheza mechi nyingi zaidi za UEFA Champions League.
CR7 kwa sasa yuko nyuma ya Ryan Giggs aliyecheza mechi 151, Xavi mechi 157 na Iker Casillas mechi 168, katika list ya UEFA ya wachezaji wa muda wote waliocheza mechi nyingi zaidi za michuano hiyo.
Huyo Ndio Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro
0 comments:
Post a Comment