Thursday, June 1, 2017

TAARIFA ZA USAJILI: Barani Ulaya


Mancini Atua Zenit
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amekabidhiwa rasmi mikoba ya kuinoa klabu ya Zenit ya nchini Urusi. Mancini anachukua nafasi ya Mircea Lucescu.

Rasmi: Huntelaar arudi Ajax
Mshambuliaji huyo anarudi katika klabu yake ya zamani ya Ajax huku akisaini dili la mwaka mmoja baada ya kuachana na Bundesliga alikokuwa anakipiga na klabu ya Schalke 04

Tetesi: Real Madrid yatenga pauni milioni 100 kuinasa saini ya Eden Hazard

Tetesi: Kruse ni miongoni mwa wanaowindwa na klabu ya Man United kwa muda na safari hii imedhamiria kuinasa saini ya straika huyo anayeitumikia klabu ya Werder Bremen.

Rasmi: Man City yakamilisha dili la pauni milioni 35 kumnasa Mlinda mlango wa Brazil Ederson

Rasmi: Villareal wakamilisha usajili wa Unal akitokea Man City kwa mkataba wa miaka mitano.

Ungana na Soka24 kwa habari za papo kwa papo za usajili kote ulimwenguni

0 comments:

Post a Comment