Thursday, June 1, 2017

Man City Yaweka Rekodi Ya Dunia Kwa Usajili Huu

Klabu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili mlinda mlango Ederson Moraes kutoka katika klabu ya Benfica ya nchini Ureno kwa kitita cha paundi milioni 35. 


Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 wa thamani hiyo ya fedha unamfanya Ederson kuwa kipa ghali zaidi kuwahi kusajiliwa kwa thamani hiyo ya pesa katika historia ya mpira wa miguu baada ya Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus akitokea Parma mnamo mwaka 2001.

Ederson alisafiri kwenda Manchester Jumatatu na Jumanne alitua katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu.
City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili kumnasa kiungo Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.

Historia yake kwa ufupi;

0 comments:

Post a Comment