Thursday, June 1, 2017

Asante Kwasi Kujiunga Na Yanga SC

Beki wa timu ya Mbao FC, Asante Kwasi amesema angetamani kuichezea Yanga katika msimu ujao wa ligi.


Beki huyo wa kati wa Mbao ameyasema hayo kutokana na kuvutiwa na kiwango na mafanikio ya klabu ya Yanga mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi soka Tanzania Bara.

Kwasi kwa sasa amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliokuwa nao katika klabu yake ya Mbao FC na ameweka wazi kuwa anapenda kujiunga na timu nyingine kubwa kama Yanga au Azam FC. Mghana huyo amedai kwa kipindi ambacho ameishi nchini amegundua kuwa Yanga ndiyo klabu yenye mafanikio hivyo kumfanya yeye kuvutiwa kucheza katika klabu hiyo.

“Yanga nimeambiwa ndiyo timu inayoongoza kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu, mara nyingi lakini pia ndiyo timu ambayo imeshiriki mara nyingi michuano ya kimataifa ukweli nimevutiwa na hilo na siku zote natamani kucheza timu yenye mafanikio kwasababu naamini ndiyo njia nyepesi ya kufika ninapopataka,”amesema Kwasi.

Beki huyo aliyeonyesha uwezo mkubwa katika msimu wa ligi uliomalizika amedai kuwa mpaka sasa bado hajajua ni timu gani ataichezea msimu ujao lakini angefurahi sana kama angetua Jangwani.

Usipitwe na habari za papo kwa papo za Usajili, Ungana na Soka24 kupata kila kinachojiri katika ulimwengu wa Soka Ulimwenguni.

0 comments:

Post a Comment