Sunday, May 14, 2017

Hull City, Middlesbrough waungana na Sunderland kushuka daraja, wakati Liverpool, Manchester City na Arsenal wanapigana kuingia nne bora ‘BIG 4’ki




Baada ya jana kukubali kichapo cha goli 2 – 1 toka kwa Southampton ndani ya Uwanja wake wa nyumbani timu ya Middlesbrough imeaga rasmi ligi kuu ya England ikiungana na Sunderland ambayo ilishashuka kitambo.

Timu ya Hull City nayo leo imenyoosha mikono juu na kuiga rasmi ligi hiyo baada ya kukubali kufungwa goli 4 – 0 na Crystal Palace na hivyo kuaga rasimi ligi.

Timu ya hull City imebakiwa na pointi zake 34 baada ya mechi 37 na imebakiwa na mchezo mmoja ambao hata ikishinda itafikisha pointi 37 ambazo timu inayoshika nafasi ya 17 ina pointi 38 tayari.

Chelsea ameshatwaa ubingwa kwa kujikusanyia pointi 87 ambazo hakuna timu yoyote inaweza kuzifikia huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi, Tottenham nayo imefanikiwa kushika nafasi ya pili ambayo timu za nyuma yake hakuna ambayo inaweza kuifikia.
Sasa mvutano mkubwa umebaki kwa timu tatu kuwania nafasi 2 za kwenda ligi ya mabingwa ulaya, timu ya Liverpool imecheza michezo 37 ina pointi 73 inafuatiwa na Manchester City iliyocheza michezo 36 ikiwa na pointi 72 huku Arsenal ikiwa imezinduka hatua za mwisho ina pointi 69 baada ya michezo 36.

Hesabu zipo hivi, kama Liverpool atashinda mchezo wake uliobaki tayari atakuwa kaingia ‘BIG 4’, Manchester City endapo itashinda mchezo mmoja kati ya miwili itakuwa imeingia ‘BIG 4’, Hesabu za Arsenal zipo hivi, kwanza ishinde mechi zake zote mbili zilizosalia halafu iombe mabaya kwa timu moja wapo kati Liverpool au Manchester City ipoteze.

Ila shida nyingine inakuja endapo Manchester United watatwaa kombe la Europa basi timu itakayoshika nafasi ya nne itabidi icheze Europa na sio kufuzu kwa ligi ya mabingwa Kutokana na sharia ya kuwa bingwa wa Europa anapata nafasi ya kuingia moja kwa moja ligi ya mabingwa.

Angalia jedwali na wewe upitishe Hesabu zako upime timu yako kama ipo kwenye huo mkondo hapo.






 matokeo ya jana jumamosi yalikuwa hivi:
Crystal Palace 4 - 0 Hull City

West Ham United 0 - 4 Liverpool
Tottenham Hotspur 2 - 1 Manchester United

 matokeo ya leo jumapili yalikuwa hivi:

Manchester City 2 - 1 Leicester City
AFC Bournemouth 2 - 1 Burnley
Middlesbrough 1 - 2 Southampton
Sunderland 0 - 2 Swansea City


Stoke City 1 - 4 Arsenal

0 comments:

Post a Comment