Friday, June 2, 2017

Simba Wapata Mbadala Wa Juuko Murshid

Munezero Fiston ni Mnyarwanda ambaye yupo katika mipango ya Simba baada ya kocha Joseph Omog kupendekeza atafutiwe mchezaji mwingine.


Munezero, anayekipiga katika klabu ya Rayon Sport anatarajiwa kutua Dar Es Salaam Jumamosi hii kwa lengo la kufanya mazungumzo na wekundu hao wa Msimbazi.

Hatua hii inakuja baada ya taarifa za kuomba kuondoka kwa beki Juuko Murshid pamoja na hali ya majeraha inayomsumbua Method mwanjali hivyo kuonekana kuna kila sababu ya kupata mbadala wa nyota hao.


“Munezero atawasili rasmi Jumamosi hii. Tunaweza kumtumia kwenye michuano ya Super Cup, mashabiki wetu watapata nafasi ya kumuona hapo,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Pamoja na beki huyo, Simba ina mpango wa kusajili wachezaji wengine watatu, ambao ni kiungo, mshambuliaji na beki mwingine kujenga ukuta imara kwenye kikosi hicho.

0 comments:

Post a Comment