Friday, June 2, 2017

Griezmann Kubaki Atletico Madrid

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amedokeza kwamba huenda asiihame klabu yake, licha ya kuwindwa na klabu  kubwa Ulaya ikiwemo Manchester United.


Mfaransa huyo wa miaka 26 aliandika kwenye Twitter: "Sasa zaidi ya zamani! #atleti #alltogether (sote pamoja)."

Alisema hayo saa chache baada ya marufuku ya kuzuia klabu hiyo kununua wachezaji kudumishwa.

Hii ina maana kwamba huenda klabu hiyo isiweze kumnunua mchezaji mwingine iwapo itamuuza.

Mnamo Alhamisi, ilibainika kwamba Manchester United nao pia wanaonekana kupunguza hamu ya kutaka kumnunua.

Kwa kuwa Atletico haiwezi kununua wachezaji wengine hadi Januari, inatarajiwa kwamba Griezmann atapewa mkataba mpya.

United walitaka sana kumnunua mshambuliaji huyo na walikuwa wanatafakari uwezekano wa kufikisha euro 100m (£87m) kumfungua kutoka kwa mkataba wake.

Lakini duru zinasema ununuzi wa Griezmann sasa si kipaumbele kwa United.
Hata hivyo endapo dili la Griezmann litashindwa kutimia bado wapo wachezaji wengine ambao United inawafukuzia akiwemo Romelu Lukaku wa Everton, Andrea Belotti wa Torino na Alvaro Morata wa Real Madrid.

0 comments:

Post a Comment