Saturday, May 13, 2017

Yanga 2 - 1 Mbeya City, Msuva akaribia kiatu cha dhahabu, yanga yaukaribia ubingwa, Majimaji yajiweka mahali salama kidogo, soma zaidi uchambuzi wa kina usisahau kulike page yetu na kujiunga na group leo



Ligi kuu Tanzania Bara 2016/17 imefikia patamu ikiwa 95% timu zote zimebakisha mchezo mmoja kivumbi kipo kuwania ubingwa na timu zinazotakiwa kushuka daraja.
Ubingwa ni mchuano wa mahasimu wa soka la bongo simba na Yanga ambapo mpaka leo hii Yanga na Simba wamefungana pointi ila Yanga anaongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, ila Yanga ina mchezo mmoja pungufu ya Simba
Simba imebakisha mchezo mmoja tu ambao utapigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa may 20 dhidi ya Mwadui
Yanga imebakisha michezo miwili mmoja dhidi ya toto jumane may 16 Uwanja wa Taifa wakati mchezo wao wa mwisho utafanyika jijini Mwanza dhidi ya Mbao FC may 20.
Uhondo upo zaidi kuwania kubaki ligi kuu baada ya Matokeo ya leo kutoa matumani kwa baadhi ya timu, Majimaji wamejifikishia pointi 32 na kujitengenzea mazingira mazuri ya kubaki endapo tu wataifunga timu ya Mbeya city may 20 huko Songea, Mbeya city yenyewe ina pointi 33.
Toto wao watamaliza ligi huko Manungu kukabiliana na timu ya Mtibwa ambayo itataka kulinda heshima tu kwani haitaki ubingwa wala haishuki daraja.
Ndana wao leo wamepigwa 2 -1 na Prisons hivyo kusalia na ponti zao 30 na watamaliza na timu ambayo ishashuka daraja ya JKT Ruvu katika dimba la Nangwanda mkoa mtwara ikishinda ponti 33.
Timu ya AfricanLyon  kesho jumapili inacheza mchezo wake wa 29 na Ruvu Shooting  huku ikwa na pointi 31ambazo si salama hata kidogo, wakati ruvu shooting nae akiwa na pointi 33.
Mechi ya mwisho may 20 African Lyon itakuwa na kibarua kizito mbele ya Prisons,

Mbio za ufungaji bora zinazidi kumkalia vizuri mshambuliaji wa timu ya Yanga Simon Msuva kwa kufikisha goli 14 huku Mbaraka Yusuf, Obrey Chirwa na Mussa wakimkaribia kwa ukaribu


MATOKEO YA LEO NI KAMA IFUATAVYO
Prisons 2-1 Ndanda
Mtibwa 4-2 Mwadui
JKT 0-1 Majimaji
Kagera 2-1 Mbao FC


0 comments:

Post a Comment