Mshambuliaji hatari wa Yanga, Amis Tambwe ametamba kuifunga tena Simba katika mechi yao inayotarajiwa kupigwa majuma kadhaa yajayo.
Tambwe mwenye magoli 9 katika ligi msimu wa 2016/17 amesema kuwa haoni beki za kumzuia katika kikosi cha Simba.
"Sijaona beki ambaye anaweza kunidhibiti nishindwe kufunga nakujua vizuri uwezo wao kwaiyo wajiandae kwa kipigo na Mimi ndio nikiwa mfungaji," amesema Tambwe.
Mrundi huyo ameongeza kuwa anajisikia furaha sana kuifunga Simba kwani ndio ndoto yake siku zote.
"Nafurahi kuona ndoto zangu zimekuwa zikitimia kwani nimezifunga Simba kwenye mechi nyingi ambazo nimekutana nayo nikiwa na Yanga,"amesema Tambwe.
Simba na Yanga zinatarajia kukutana Februari 25.
0 comments:
Post a Comment