Thursday, February 9, 2017

Leicester City Yatinga Raundi ya 5 FA CUP

Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima katika uwanja wake wa nyumbani wa king power kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Derdy County katika michuano ya  FA CUP away mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya michuano hiyo.

Hadi dakika 90 za mchezo zina maliziaka timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-1 na kulazimia kuongezwa kuda wa ziada.

Leiceister city ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Andy King ,na baadaye Derdy County wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Abdoul Camara, huku Onyinye Wilfredy Ndindi akiongeza bao la pili kwa upande wa Leceister city katika dakika ya 94 muda wa nyongeza.

Dakika ya 114 Demaria Gray akapigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Derby County kwa kuandika bao la tatu na la mwisho.

Kwa matokeo hayo sasa Leiceister city watakutana na Milwall katika raundi ya tano wakiwa ugenini.

0 comments:

Post a Comment