Tuesday, August 30, 2016

OMOG ASHUSHA PRESHA ZA WANAMSIMBAZI

Kocha wa klabu ya Simba, Mcameroon, Joseph Omog amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kufuatia sare ya bila kufungana waliyoipata dhidi ya JKT Ruvu.

Omog amesema hayo ni matokeo ya kawaida ya kimchezo hivyo mashabiki na wanachama wasiwe na wasiwasi.

“Najua wanasimba wana kumbukumbu ya msimu uliopita ambapo timu yao haikuwa ikifanya vizuri katika mechi zake huu ni msimu mwingine na nawahakikishia matokeo yatakuwa mazuri tu,” alisema Omog.

“Lakini lazima watu wajue kuwa Simba ni timu kubwa hivyo kila mtu akikutana nayo anataka kuifunga, tusikatishwe na matokeo ya sare ni kawaida tu,” aliongeza Kocha huyo.

Mashabiki wa Simba wanasumbuliwa na kumbukumbu mbaya ya msimu uliopita ambayo ilishuhudiwa klabu hiyo ikikosa hata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu, hivyo matokeo yoyote mabaya kwa kiasi fulani yanaleta huzuni kubwa kwa wapenzi wa klabu hiyo, lakini kocha Omog amesema anaamini makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu yatarekebishwa na klabu itafanya vizuri na kuibuka na ushindi mkubwa katika mechi ijayo.

===========
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm

Nyota Wa Zamani Wa Man U Aitabiria Ubingwa Chelsea


Aubameyang Aitamani Real Madrid


Simba Yabadili Gia Angani

Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

Related Posts:

  • FARID MUSSA ATUA JIJINI DAR Farid Mussa Mchezaji Wa Timu Ya Azam FC Amewasili Jijini Dar Akitokea Hispania Alikokwenda Kufanya Majaribio Ya Kucheza Soka La Kulipwa Katika Klabu Ya Deportivo Tenerife Farid amewasili salama jijini Dar jana majira ya … Read More
  • HAYA NDO ALIYOAHIDIWA KOCHA PLUIJM YANGA Mkataba wa kocha mkuu wa Yanga Hans Pluijm ukiwa umebakiza siku chache kumalizika Yanga yafunguka juu ya kuendelea kubaki na kocha huyo. Klabu ya Yanga imeanza mazungumzo rasmi na kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm… Read More
  • MBAO FC YAAHIDI MAKUBWA LIGI KUU Timu ya Mbao FC iliyopanda daraja Kufuatia maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF ya kuzishusha daraja timu 4 za kundi C na kuifanya Mbao kushika nafasi ya kwanza katika kundi hilo..Imeahidi kuwashangaza wapenda soka katika lig… Read More
  • DENIS KITAMBI KATIKA MTIHANI MZITO AZAM FC Kocha Msaidizi wa Azam FC  Denis Kitambi Ataiongoza klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa Ligi katika kuwania nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara. Ligi Kuu Tanzania Bara inaelekea ukingoni na mechi… Read More
  • SAKATA LA STAND UNITED KUWA KAMPUNI LAZIDI KULETA UTATA Wanachama na Mashabiki wa klabu ya Stand United Wamepinga suala ya timu yao kuendeshwa kama kampuni. Siku Chache zilizopita Soka24 ilikuletea taarifa juu ya kampuni ya ACACIA inayoidhamini klabu ya Stand United kutishia … Read More

0 comments:

Post a Comment