Saturday, July 23, 2016

MEDEAMA YAICHIMBA MKWARA YANGA

Klabu ya Medeama SC imetoa onyo kwa Yanga kuelekea mchezo wao wa marudiano utakaofanyika siku ya Jumatano huko nchini Ghana.

Mkwara huo umekuja baada ya Medeama kushinda katika mchezo wake dhidi ya Liberty Professionals wa goli 1 - 0 huku wakionyesha mchezo safi kabisa.
Kitendo hicho cha Medeama kushinda katika mchezo huo kumewaongezea hamasa kuelekea mchezo wao na Yanga utakaopigwa kwenye dimba la Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi.

Yanga ilitoa sare ya kufungana 1 - 1 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na kuifanya Yanga izidi kushika nafasi ya mwisho katika Group A ambalo linaongozwa na TP Mazembe.

Ushindi huo dhidi ya Liberty umeifanya Medeama kufika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imebaki na mchezo mmoja mkononi. Timu hiyo imepoteza mechi moja tu kwenye Uwanja wa Tarkwa na Aboso Park, ikishinda mabao 13 na kutoka sare mara mbili.

Wapinzani hao wa Yanga wana imani ya kusonga mbele baada ya kupoteza mchezo mmojana kutoka sare mbili katika mzunguko wa kwanza hatua ya makundi na hivyo, wakiwa na pointi mbili, huku Yanga ikishika mkia kwa pointi moja, TP Mazembe na Mo Bejaia zikiongoza.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans-van-der-Pluijm amesema ni lazima wacheze kwa kujitoa ili kupata matokeo mazuri.

“Tunahitaji kuwa wa kipekee kwa kucheza mchezo wa pasi nyingi. Tunajisikia huru tukiamini kuwa tunaweza kubadilisha matokeo,” alisema.

Mchezo wa Yanga utafanyika kuanzia saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki huku TP Mazembe wakicheza na Bejaia nchini Congo siku hiyo hiyo katika mchezo utakaoanza mapema.
Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni.

0 comments:

Post a Comment