Saturday, July 23, 2016

SUNDERLAND YAMRUDISHA DAVID MOYES UINGEREZA

Klabu ya Sunderland imemteua kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya Sam Allardyce kukabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya England.

Moyes anachukua mikoba ya Sam Allardyce katika dimba la Stadium Of Light. Moyes amesaini mkataba wa miaka minne na Paka hao Weusi na alionekana kuwa chaguo la mwenyekiti wa klabu hiyo Ellis kwa muda mrefu.

Moyes 53, aliyekatimuliwa na klabu ya Man United mara tu baada ya kukabidhiwa mikoba kufuatia kuondoka kwa kwa Alex Ferguson na kuwa na wakati mgumu na klabu hiyo bado yuko Hispania na klabu ya Real Sociedad kwa sasa na ataanza majukumu ya kuiongoza Sunderland msimu ujao.
Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni.

Related Posts:

  • Tetesi Mpya Za Usajili Manchester United Tetesi za usajili katika klabu ya Manchester United. Man United Kukamilisha Uhamisho Wa Lacazette klabu ya Manchester United ipo mbioni kuhakikisha inamsajili straika wa Lyon Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa L'Equipe … Read More
  • Tetesi Mpya Za Usajili Arsenal Ungana na Soka24, kwa habari za papo kwa papo za usajili katika klabu kubwa na pendwa zaidi duniani, hapa nimekuwekea yanayojiri katika klabu ya Arsenal hivi sasa. Arsenal katika mbio za Kumuwania Mbappe klabu ya Arsenal… Read More
  • Tetesi Mpya Za Usajili Liverpool Klabu ya Liverpool imefuzu kushiriki michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya UEFA Champions League msimu ujao wa 2017/18. Kuelekea katika michuano hiyo na ligi kuu nchini England, klabu hiyo imeshaanza kuziwania saini za wach… Read More
  • Yote Yanayoihusu Azam FC;Usajili, Waliotemwa Wanaoingia Na Mipango Msimu Ujao UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifu wapenzi na mashabiki wa soka nchini kuwa imebadilisha mfumo wa usajili uliokuwa ikiutumia awali wa kusajili wachezaji kwa gharama kubwa na s… Read More
  • PSG Wakubali Yaishe Kwa Aubameyang Vigogo wa soka nchini Ufaransa, PSG wamekubali kutoa paundi milioni 61 kuinasa saini ya mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Licha ya gharama hizo za uhamisho PSG pia wamekubali kumlipa nyota huyo kutoka b… Read More

0 comments:

Post a Comment