Sunday, June 5, 2016

SAMATTA AIPA YANGA MBINU ZA KUIMALIZA TP MAZEMBE

Mchezaji wa zamani wa klabu ya TP Mazembe ya Congo, Mbwana Ally Samatta amesema Inawezekana Yanga kuifunga TP Mazembe


Samatta anayecheza katika klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji ameonyesha kufurahishwa kwake baada ya timu ya Yanga kutinga hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika na amesema inawezekana kabisa kwa Yanga kuifunga timu yake ya zamani TP Mazembe.

Samatta amesema kikubwa ni Yanga kujipanga vizuri kabla hawajakutana na vigogo hao wa soka Afrika na kuhakikisha wanapambana kikamilifu pale watakapokutana.

"Inawezekana kabisa Yanga kuifunga Mazembe lakini kama watajipanga vizuri kwa sababu mpira unabadilika na chochote kinaweza kutokea ilimradi wacheze kwa malengo" alisema Mbwana Samatta.

Akielezea kitendo cha Yanga kufika hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika, amesema hatua hiyo ni nzuri kwa maendeleo ya soka la Tanzania na itasaidia kutangaza mpira wa Tanzania na kuleta hamasa kubwa kwa wachezaji wa ndani kujituma zaidi.

Yanga imepangwa kundi moja na TP Mazembe, Medeama na MO Bejaia, na itacheza na TP Mazembe kati ya Juni 28 na 29.

0 comments:

Post a Comment