Sunday, June 5, 2016

HUYU NDO ANAETARAJIWA KUCHUKUA MIKOBA YA KOCHA JACKSON MAYANJA SIMBA

Simba ipo katika harakati za kukisuka upya kikosi chao na tayari wapo katika mazungumzo na kocha Mzimbabwe Kalisto Pasuwa.




Mwenyekiti wa kamati ya Usajili Simba Zacharia Hans Pope yupo katika mazungumzo ya mwisho na kocha huyo kwa ajili ya kuja kuchukua mikoba ya kocha Mayanja katika klabu ya Simba.
Hans Poppe ameonyesha uhakika wake juu ya kocha huyo kutua Simba huku akisema kuwa Pasuwa tayari ameshakubali ofa aliyopewa na klabu ya Simba hivyo kuwataka wanasimba kuwa watulivu wakati harakati za kuimarisha kikosi chao zikiendelea.

"Ni Kocha mwenye uwezo mkubwa ndiyo maana taifa lake likamuamini na kumpa timu ya taifa, ujio wake tunaamini ataweza kuvunja nguvu za wachezaji wa Yanga Donald Ngoma na Thabani  Kamusoko" yalikuwa maneno ya Hans Pope.

Aidha Hans alisema wapo katika mazungumzo pia na mshambuliaji hatari kutoka huko huko nchini Zimbabwe ambaye naye pia anaitumikia timu yake ya taifa ya Zimbabwe lakini hakumtaja kwa jina.

0 comments:

Post a Comment