Ibrahimovic amesema mechi yake ya mwisho ni kati ya Sweden na Ubelgiji itakayochezwa Jumatano. Sweden itacheza na Ubelgiji jumatano hii huku wakiwa na pointi 2 tu katika michezo waliyocheza wakiwa nyuma ya wapinzania wao waliopo katika nafasi ya pili katika kundi lao.
"Mechi ya mwisho ya Sweden kwenye michuano ya Euro itakuwa ndiyo mechi yangau ya mwisho kwa nchi yangu" alisema Ibrahimovic alipozungumza na waandishi wa habari.
"Hivyo mechi yangu ya mwisho ya Euro ndiyo ya mwisho. Tuombe kudumu kwenye michuano hii kwa muda. Natumai mechi ya kesho (leo) haitakuwa mechi yangu ya mwisho, lakini sina majuto yoyote." aliongeza Mkongwe huyo anayehusishwa kujiunga na Mashetani Wekundu chini ya kocha Mourinho.
Ibrahimovic aliongeza kuwa hajavunjika moyo kwa jambo lolote na kwamba anajivunia kwa nahodha wa Sweden. Alitumia nafasi hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kutoa shukrani zake kwa mashabiki wote kwa ushirikiano waliompa na kusisitiza kuwa daima yeye atasimama imara kuibeba bendera ya Sweden.
0 comments:
Post a Comment