Wednesday, May 25, 2016

MNAOSUBIRI MOURINHO KUTANGAZWA KUWA KOCHA WA MAN U, HIKI NDO KINACHOCHELEWESHA DILI HILO

Van Gaal ameshafukuzwa Manchester United na Matarajio ya wengi ni kusikia Mourinho akitangazwa kurithi mikoba ya Mholanzi huyo lakini kumekuwa na sababu ambayo inachelewesha Mourinho kutangazwa Rasmi.



Usajili wa Mourinho Man U unakaribia kukamilika kwa kiasi kikubwa ila kuna mambo kidogo ambayo hayajakaa sawa yanayofanya suala hilo kuchelewa. Usiku wa jana Sky Sports iliripoti kuwa Mourinho ameshafikia makubaliano na United kwa dili hilo kutangazwa rasmi saa 24 hadi 48 zijazo. Wakala wa Mourinho Jorge Mendes amezungumzia maendeleo ya uhamisho huo wa Mourinho huku akisema kila kitu kimekamilika,kitu kinacholeta shida kidogo ni kwamba Chelsea klabu ya zamani ya Mourinho inamiliki haki ya alama/nembo ya Biashara (Trademark) pamoja na haki za picha za Mourinho kitu ambacho kinatafutiwa muafaka kwa sasa.

Mwanasheria wa Mourinho pia aliyasema hayo alipoulizwa juu ya kuchelewa kwa dili hilo.
Cohen alisema hiki si kitu cha kawaida katika mkataba wa ajira na kwamba Mourinho alishauriwa sana asifanye maamuzi hayo wakati anaingia mkataba na Chelsea mara baada ya kutimuliwa Madrid lakini ilishindikana,  na kitu hicho ndo kinaleta mgongano wa kimaslahi kati yake na waajiri wake wa zamani. Mourinho ana udhamini katika kampuni ya utengenezaji wa magari ya Jaguar huku Manchester wao wakidhaminiwa na mpinzani wa Jaguar katika magari kampuni ya Chevrolet.


Hatahivyo hili haliwezi kuwa tatizo kubwa la kuzuia United kumnasa kocha huyo na kwamba mambo yanaendelea kuwekwa sawa na inatarajiwa Alhamisi au Ijumaa Mourinho kutangazwa rasmi kuwa kocha wa Man United.

Kumiliki nembo ya biashara na haki ya picha ya Mourinho maana yake ni kwamba Chelsea wanahaki ya  kuingia mikataba na makampuni kupitia nembo ya Mourinho aidha kwa kutumia jina lake au Picha yake licha ya kutokuwepo klabuni hapo.

Related Posts:

  • DAVID MOYES AWANASA WAWILI KUTOKA MANCHESTER UNITED Boss Mpya wa klabu ya Sunderland, David Moyes amekamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka katika klabu ya Manchester United. Klabu ya Manchester United imethibitisha kuuzwa kwa wachezaji wao wawili ambao ni Paddy McNa… Read More
  • SUNDERLAND YAMRUDISHA DAVID MOYES UINGEREZA Klabu ya Sunderland imemteua kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya Sam Allardyce kukabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya England. Moyes anachukua mikoba ya Sam Allardyce k… Read More
  • VIDEO: INTERVIEW YA KWANZA YA DAVID MOYES SUNDERLAND David Moyes ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Sunderland akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sam Allardyce aliyekabidhiwa timu ya taifa ya Uingereza. Hii hapa chini Interview Yake ya kwanza mara tu baada ya kutang… Read More
  • RASMI: MANCHESTER CITY YAMNASA MORENO Klabu ya Manchester City iliyo chini ya kocha Mpya Pep Guardiola imekamilisha uhamisho wa kinda Mkolombia Marlos Moreno. Moreno 19, ametua katika dimba la Etihad akitokea Atletico Nocional na amesaini mkataba wa miaka mit… Read More
  • CLAUDIO RANIERI AIONYA MAN UNITEDClaudio RanieriKocha Wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza Leicester City, Claudio Ranieri ameionya Man United kuwa wasitegemee mchezo rahisi leo. Ranieri amedai anaamini kuna kitu kizuri kinakuja katika klabu yak… Read More

1 comments: