Wednesday, May 25, 2016

HAYA NDO MAAMUZI YA RAFA BENITEZ BAADA YA NEWCASTLE KUSHUKA DARAJA

Kocha wa klabu ya Newcastle United ya Nchini Uingereza ambayo imeshuka daraja rasmi na kwenda kutafuta nafasi ya kurudi ligi kuu katika ligi daraja la kwanza ameweka wazi maamuzi yake kwa klabu hiyo.


Habari kubwa kwa wepenzi na mashabiki wa Newcastle United ni kwamba Kocha Rafa Benitez amekubali kubaki klabuni hapo licha ya timu hiyo kushuka daraja. Benitez tayari ameshasaini mkataba wa miaka mitatu utakaoendelea kumuweka klabuni hapo. Benitez alipewa kibarua cha kuinoa Newcastle United baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtupia virago Steve McClaren aliyekuwa kocha mkuu kwa kipindi hicho.



Katika mkataba wake na Newcastle Benitez alikuwa huru kuondoka klabuni hapo endapo klabu hiyo itashuka daraja na kinyume na ilivyotarajiwa na wengi kwamba Benitez angeondoka klabuni hapo mara baada ya Newcastle kuwa imeshuka daraja, yeye mwenyewe ameamua kumwaga wino na kuendelea kubaki.

0 comments:

Post a Comment