Van Gaal ameshafukuzwa Manchester United na Matarajio ya wengi ni kusikia Mourinho akitangazwa kurithi mikoba ya Mholanzi huyo lakini kumekuwa na sababu ambayo inachelewesha Mourinho kutangazwa Rasmi.
Usajili wa Mourinho Man U unakaribia kukamilika kwa kiasi kikubwa ila kuna mambo kidogo ambayo hayajakaa sawa yanayofanya suala hilo kuchelewa. Usiku wa jana Sky Sports iliripoti kuwa Mourinho ameshafikia makubaliano na United kwa dili hilo kutangazwa rasmi saa 24 hadi 48 zijazo. Wakala wa Mourinho Jorge Mendes amezungumzia maendeleo ya uhamisho huo wa Mourinho huku akisema kila kitu kimekamilika,kitu kinacholeta shida kidogo ni kwamba Chelsea klabu ya zamani ya Mourinho inamiliki haki ya alama/nembo ya Biashara (Trademark) pamoja na haki za picha za Mourinho kitu ambacho kinatafutiwa muafaka kwa sasa.
Mwanasheria wa Mourinho pia aliyasema hayo alipoulizwa juu ya kuchelewa kwa dili hilo.
Cohen alisema hiki si kitu cha kawaida katika mkataba wa ajira na kwamba Mourinho alishauriwa sana asifanye maamuzi hayo wakati anaingia mkataba na Chelsea mara baada ya kutimuliwa Madrid lakini ilishindikana, na kitu hicho ndo kinaleta mgongano wa kimaslahi kati yake na waajiri wake wa zamani. Mourinho ana udhamini katika kampuni ya utengenezaji wa magari ya Jaguar huku Manchester wao wakidhaminiwa na mpinzani wa Jaguar katika magari kampuni ya Chevrolet.
Hatahivyo hili haliwezi kuwa tatizo kubwa la kuzuia United kumnasa kocha huyo na kwamba mambo yanaendelea kuwekwa sawa na inatarajiwa Alhamisi au Ijumaa Mourinho kutangazwa rasmi kuwa kocha wa Man United.
Kumiliki nembo ya biashara na haki ya picha ya Mourinho maana yake ni kwamba Chelsea wanahaki ya kuingia mikataba na makampuni kupitia nembo ya Mourinho aidha kwa kutumia jina lake au Picha yake licha ya kutokuwepo klabuni hapo.
mnajitahidi mko vizuri
ReplyDelete