Monday, May 23, 2016
HUYU NDO ATAKAE AMUA FAINALI FA CUP KATI YA YANGA NA AZAM FC
Mwamuzi mahiri nchini, Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam, Jumatano Mei 25, 2016 ameteuliwa kuwa mwamuzi atakayechezesha mchezo wa fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayozikutanisha timu za Young Africans na Azam FC; zote za jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza kesho saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand Chancha wa Mwanza (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam (line 2) na mwamuzi wa akiba mezani ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia. Kamishna wa mchezo huo anatakuwa Juma Mgunda wa Tanga.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu msimu 2015/16, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu 2015/16 wataiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2016/17. Nafasi hiyo imechukuliwa na Young Africans.
Kadhalika Azam ina tiketi tayari ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kufika fainali za ASFC ingawa kanuni zinataka bingwa ambako kwa upande wa Yanga wana tiketi ya michuano ya juu zaidi ya shirikisho. Mvuto wa mchezo wa Jumatano ni ushindani wa soka na zawadi kwa bingwa.
Fainali za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
Related Posts:
LIVE: MECHI ZA KUWANIA NAFASI YA PILI, AZAM FC 1-1 MGAMBO JKT, SIMBA SC 1 - 2 JKT RUVU LIGI KUU TANZANIA BARA MECHI ZA KUWANIA NAFASI YA PILI FULL TIME Azam FC 1 - 1 Mgambo JKT Simba SC 1 - 2 JKT Ruvu MSIMAMO KWA SASA POSITION TEAM PLAYED GD POINTS 2 … Read More
KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA JKT RUVU HIKI HAPA Kikosi cha akiba ni 1. Vicent Angban2. Said Issa3. Mohamed Mussa4. Hussein Magila5. Fredy Antony6. Said Hamis … Read More
MOHAMED TSHABALALA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MARCH Mchezaji Mohamed Tshabalala ameshinda tunzo ya mchezaji bora kwa mwezi wa March - April 2016. … Read More
HABARI ZOTE KUBWA ZA MICHEZO MAGAZETINI LEO MEI 23, 2016 Soma Vichwa Vya Habari Za Michezo Magazetini Kila Siku Asubuhi Kupitia Hapa Soka24.blogspot.com … Read More
MASHABIKI YANGA WACHOMA MOTO MAGAZETI YA THE GUARDIAN NA NIPASHE Wanachama na mashabiki wa Yanga wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na IPP MEDIA Wanachama hao walionekana kukasirishwa na kitendo cha Reginald Mengi kutumia vyombo … Read More
0 comments:
Post a Comment