Monday, May 23, 2016

WAAMUZI 40 KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA MIKOA (RCL)

Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeteua waamuzi 40 watakaochezesha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL) inayoanza leo Mei 23 katika vituo vinne tofauti hapa nchini.


Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27, imegawanywa katika makundi manne ambako bingwa katika kila kundi atapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 ngazi ya taifa kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza Ligi daraja la Kwanza msimu wa 2017/18.

Timu tano zitapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili ambako mbali ya washindi katika vituo vyote vinne, mshindwa bora katika vituo vya Njombe, Morogoro na Singida nayo itapanda daraja kwa kuangalia vigezo vya wingi wa pointi, wastani wa mabao, mabao kufunga na mabao ya kufungwa. Kituo cha Kagera hakijajumuishwa kwa kuwa kina timu shiriki sita.

Waamuzi walioteuliwa kuchezesha ligi hiyo kwa kituo cha Njombe ni Elasto Msaliwa, Klement Manga, Mashaka Lulambo, Lazaro Mbogoro, Michael Mkongwa, Alex Chitalula, Maulid Makiwa, Michael Kilango, Edina Ndelwa na Haidal Kisingile.

Timu zinazoshiriki ni Mkali Stars ya Ruvuma, Mtwivila (Iringa), Sido FC (Mbeya), Jangwani FC ya Rukwa, Nyundo FC ya Katavi, Mawezi ya Morogoro na Zimamoto ya Ilala, Dar es Salaam.

Kituo cha Morogoro walioteuliwa ni Athuman Lazi, Mohammed Theophil, Seleman Kinugane, Fikiri Yusuph ‘Magari’, Nicolaus Makangara, Mwarabu Mumba, Emmanuel Muga, Herry Shao, Shaban Juma na Makongo Katuma na timu zinazoshiriki ni Stend  FC ya Pwani, Mbuga FC (Mtwara), Namungo FC(Lindi), Muheza United ya Tanga, Stand Misuna FC ya Singida, Makumbusho ya Kinondoni na Sifa Politan SC ya Temeke, Dar es Salaam.

Kituo cha Singida wako Meshack Suda, Abdallah Mwinyimkuu, Sarah Bongi, Lucas Mathias, Amani Mwaipaja, Siyachitema Kawinga, Theophil Tegamaisho, Shaaban Msangi, Aboubakar Irume na Frederick Ndahani na timu shiriki ni Veyula FC (Dodoma), Pepsi SC (Arusha), Kitayosce FC (Kilimanjaro), Stand FC (Tabora), Murusagamba FC (Kagera), Fire Stone (Manyara) na Tomato FC (Njombe).

Kituo cha Kagera walioteuliwa ni Jonesia Rukyaa, Jamada Ahmada, Ringston Rwiza, Grayson Buchard, Grace Wamala, Edgar Lyombo, Yahaya Juma, Adrian Karisa, Getrude Kahawa na Ahmada Simba na timu shiriki ni Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela City (Shinyanga), Ambassador FC (Simiyu), Igwe FC (Mara) na Mashujaa (Kigoma).

Related Posts:

  • TFF YATOA ONYO KALI KWA VILABU LIGI KUU Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa onyo kali kwa timu zote kutojiingiza kwenye mtego wa aina yoyote wa kupanga matokeo. Wakati pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara likitarajiwa kufungwa Jumapili Mei 22, 20… Read More
  • YANGA; "KOMBE LA UBINGWA LIGI KUU HALINA HADHI" Ofisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amelikosoa kombe la ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kusema halina Hadhi. Akizungumza na waandishi wa Habari jana Muro alisema kombe hilo halina hadhi ukilinganisha na uku… Read More
  • HIZI NDO SABABU ZILIZOPELEKEA AZAM FC KUPOKWA POINTI 3 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepitia marejeo ya uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kuipoka pointi zake ilizovuna kutoka mchezo Na. 156 dhidi ya Mbeya City ya Mbeya katka mchezo uliofanyika Uwanja wa soko… Read More
  • WAHISPANIA WAMWAGA WINO AZAM FC Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, tayari umefikia makubaliano na wakufunzi kutoka  nchini Hispania, Kocha Mkuu Zeben Hernandez na Mtaalamu wa Viungo, Jonas Garcia. Makocha hao wawili wa… Read More
  • SERENGETI BOYS YATINGA NUSU FAINALI Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 19, 2016 imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini  Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wen… Read More

0 comments:

Post a Comment