Tuesday, May 24, 2016

CAF YAITUPA AS VITA NJE YA MASHINDANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

Klabu ya AS Vita ya nchini Congo imeondolewa katika michuano ya Klabu bingwa Afrika baada ya kumchezesha Idrissa Traore ambaye hakustahili kucheza na nafasi yao sasa itachukuliwa na timu ya Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini.

AS Vita ilimchezesha Idrissa Traore ambaye alifungiwa kucheza mechi 4, Traore alitumikia adhabu hiyo katika mchezo mmoja tu na alikuja kucheza na Mafunzo FC ya visiwani Zanzibar.

Sheria za shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika zinasema Timu ya mwisho itakayocheza na timu ambayo mchezaji wao amefungiwa ndio itakayopewa nafasi ya timu iliyofanya kosa hilo. Mechi ya mwisho ya AS Vita ilikuwa ni dhidi ya Mamelodi Sundowns katika michuano ya klabu bingwa Afrika mchezo ambao uliisha kwa sare ya 2 - 2 lakini Sundowns wakaondolewa kwa sheria za goli la Ugenini, kwakuwa Sundowns ndo timu ya mwisho kucheza na AS Vita basi bahati imewaangukia wao na watarudi tena katika michuano ya klabu bingwa afrika.

Taarifa zaidi itakujia..............

0 comments:

Post a Comment