Tuesday, May 24, 2016

CHRISTIANO RONALDO HATARINI KUIKOSA FAINALI UEFA CHAMPIONS

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Christinao Ronaldo amegongana na Kiko Casilla katika mazoezi leo asubuhi, kugongana ambako kulimpelekea CR7 kutoka nje kitu ambacho kimeleta hofu juu ya uwepo wake katika fainali ya klabu bingwa ulaya.

Ronaldo akiwa anaugulia maumivu baada ya kugongana na Kiko


Christiano Ronaldo ameacha hofu kwa mashabiki wa Bernabeu baada ya kupata majeraha hayo, Madrid walikuwa wanafanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa fainali utakaochezwa Jumamosi hii San Siro dhidi ya mahasimu wao wa jiji moja Atletico Madrid ndipo Ronaldo alipogongana na mlinda mlango huyo na kutoka nje ya uwanja.




Hata hivyo tukio hilo halijaonekana kuwa kubwa sana lakini inaweza ikaleta shida kwa Zidane anayehitaji kuweka historia mpya katika maisha yake ya ukocha.

0 comments:

Post a Comment