Tuesday, May 24, 2016

SIMON MIGNOLET APATA MPINZANI MPYA LIVERPOOL

Klabu ya Liverpool imefikia makubaliano na mlinda mlango wa Klabu ya Mainz Loris Krius na tayari mlinda mlango huyo ameshafuzu vipimo vyake.
 
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anakijenga upya kikosi chake baada ya kufikia makubaliano na golikipa wa Mainz Loris Karius.

Loris 22, kwa sasa yupo jijini London katika kukamilisha dili la Paundi milioni 4.7 kama ada ya uhamisho wake kutoka Mainz na tayari alishafanyiwa vipimo na matokeo yamekuja vizuri.

Karius, anakuwa mchezaji wa 3 kusajiliwa na Klopp klabuni hapo baada ya kumnasa Joel Matip na Marko Grujic.

Kusajiliwa kwa mlinda mlango huyo kutaleta changamoto kwa Simon Mignolet ambaye amekuwa akinyooshewa vidole mara nyingi kutokana na kiwango chake.



0 comments:

Post a Comment