Saturday, May 7, 2016

BAYERN MUCHEN MABINGWA BUNDESLIGA 2015/16



Bayern Muchen wametwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuichapa Ingolstadt kwa jumla ya magoli 2 - 1. Bayern wametwaa ubingwa huo kwa mara ya 27 katika ligi kuu ya Nchini Ujerumani. Magoli yaliyofungwa dakika ya 15 na 32 na mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Lewandowski yametosha kuipa ushindi Bayern huku Lewandowski mwenyewe akiwa katika chati ya Wafungaji bora wa ligi hiyo akiwa amefunga magoli 29 katika ligi huku akifuatiwa na Aubameyang wa Borussia Dortmund aliyepachika magoli 25.

Matokeo Mengine Mechi za Leo May 7,Ligi kuu Ujeruman- Bundesliga.

M'gladbach 2 - 1 Bayer Leverkusen

Frankfurt 1 - 0 Dortmund

Hamburger SV 0 - 1 Wolfsburg

Hannover 96 1 - 0 Hoffenheim

Hertha 1 - 2 Darmstadt

Köln 0 - 0 Werder Bremen

Schalke 04 1 - 1 Augsburg


Stuttgart 1 - 3 Mainz

0 comments:

Post a Comment