Mbunge wa Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (Cuf), Katani Ahmad Katani ametoa kitita cha Sh 500,000 kwa wachezaji wa Ndanda FC baada ya kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam FC, leo.
Ndanda FC imeonyesha si laini baada ya kuilazimisha sare ya mabao 2-2 Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Katani amesema amefurahishwa na Ndanda na pia kuahidi kutoa Sh milioni moja kwa kila mechi ambayo Ndanda watashinda.
“Pia nitanunua kila bao watakalofunga kwenye mechi zao, Ndanda ni timu ya mkoa wa Mtwara ambako ninatokea.
Ninafanya hivi kuwahamasisha vijana ili wapambane zaidi,” alisema Katani.
Ndanda ilionyesha soka la kuvutia katika kipindi cha pili wakati wa mechi yao dhidi ya Azam FC leo na kusawazisha mabao yote mawili baada ya wenyeji wao kutangulia kwa kuwafunga mabao mawili.
Wednesday, April 6, 2016
NDANDA FC WAMIMINIWA MIPESA BAADA YA SARE NA AZAM FC
Related Posts:
George Lwandamina Aifungukia Simba SC Kocha wa mabingwa soka Tanzania bara Timu ya Yanga Mzambia George Lwandamina ametamba kwamba mechi dhidi ya timu ya Ngaya Club ya Comoro katika mchezo wa klabu bingwa afrika zitawapa taswira nzuri kabla ya kuvaana na maasimu… Read More
Simba yajifua Zanzibar kuelekea february 25 Timu ya Simba jana imeondoka kwenda visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wake wa February 25 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga. Simba ambayo ndio inayoongoza ligi kwa kujikusanyia point 51 katika michezo 22, watani z… Read More
Jamhuri Kihwelu "Julio" Aomba Kibarua Simba Kocha mkuu wa zamani wa klabu ya Mwadui ya mjini Shinyanga, Jamhuri Kihwelu, ameweka bayana kuwa yupo tayari kurudi kuitumikia Simba katika nafasi ya ukatibu mkuu. Julio amesema kuwa hana wasiwasi na yupo tayari kuitumiki… Read More
Rungu La TFF Latua Kwa Hemed Morocco Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Morocco kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000. atika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu z… Read More
Kaseja mchezaji bora ligi kuu Tanzania Bara mwezi January … Read More
0 comments:
Post a Comment