Friday, April 8, 2016

Joseph Kimwaga Ajutia Kutua Msimbazi


kimwaga Kushoto akishangilia goli
Sraika wa Simba, Joseph Kimwaga ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ya soka, basi ni kutua kuichezea timu hiyo.

Mshambuliaji huyo alitua kuichezea Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Azam FC kwa mkopo, ambapo amekuwa haonekani Simba kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kutokana na kutokea sintofahamu kati yake na uongozi.

 Kimwaga alisema alitarajia kufanya mengi makubwa akiwa na Simba, lakini ndoto zake zilikatishwa baada ya kutopewa nafasi ya kucheza.

Amesema Simba ndiyo waliyoifuata Azam kumuomba kwa mkopo na moja ya makubaliano ni kupata nafasi ya kucheza ili akuze zaidi kiwango chake, lakini baada ya kutua mambo yakabadilika.

“Sikutarajia kuyaona haya ninayoyaona hivi sasa Simba, kiukweli siamini, hivyo nimeona ni bora nikae nje ya timu ili nitulize akili yangu kuliko niwe ndani ya timu bila faida.

“Ninajuta kukubali kuja kuichezea Simba, inafikia kipindi ninafikiria vitu vingi sana kwa timu iliyokufuata wenyewe kukuomba kwa mkopo ukakubali halafu baadaye wanafanya vitu sivyo kabisa.

“Nimeona niwaachie timu yao na mimi nifanye mambo yangu mengine huku nikisubiria mkataba wangu miezi mitano na Azam kumalizika, kwa sababu nilifanya kila ninaloliweza ili nipate namba lakini nikashindwa,” alisema Kimwaga.

SOURCE: CHAMPIONI

Related Posts:

  • PAUL NONGA ANYOOSHA MIKONO YANGA Mchezaji aliyejiunga na Yanga akitokea Stand United Paul Nonga amesema ameuomba uongozi wa Yanga umuuze. Nonga amefikia uamuzi huo baada ya kukosa nafasi ya kucheza muda mwingi katika klabu hiyo. ”Nimeomba kuuzwa na tay… Read More
  • MUNAODHANI KIPRE TCHETCHE ATAJIUNGA NA YANGA, HII NDO KAULI YAKE KWENU Mchezaji Kipre Herman Tchetche amesema hana mpango wa kujiunga na klabu nyingine yoyote ya Tanzania. Tchetche amefikia hatua ya kuyazungumza hayo kufuatia uvumi unaotawala hivi sasa ukimuhusisha yeye kujiunga na klabu ya… Read More
  • AL AHLY WAMNYATIA DONALD NGOMA Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma ameanza kuwindwana vigogo wa soka la Misri na Afria timu ya Al Ahly. Ngoma amekuwa mshambuliaji tishio sana katika klabu ya Yanga na ametoa mchango mkubwa sana katika ma… Read More
  • TWIGA STARS KUVAANA NA RWANDA Timu ya soka Taifa ya Wanawake ya Tanzania – Twiga Stars, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rwanda, utakaofanyika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda. Rwanda wameomba mchezo ufanyike ili ku… Read More
  • KIPRE TCHETCHE AOMBA KUONDOKA AZAM FC Kipre Tchetche mchezaji wa Azam FC raia wa Ivory Coast amesema inatosha sasa kucheza Tanzania hivyo anataka kwenda kujaribu sehemu nyingine. Kipre ambaye ana mwaka mmoja umebaki katika mkataba wake ametosheka na muda ali… Read More

0 comments:

Post a Comment