Kocha Mkuu wa Yanga |
YANGA inajiandaa kufungasha virago vyao kutoka Kisiwani Pemba ilipoenda kujichimbia kwa siku chache kujiandaa na mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ikiwa huko Vijana wa Jangwani wamepewa mbinu fulani za kimafia.
Mbinu hizo walizopewa vijana hao wa Jangwani wana lengo la kuzitumia kwenye mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Al Ahly ya Misri ili kurahisisha mipango ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo yenye zawadi ya mamilioni ya fedha
Mabingwa hao wa Tanzania walijichimbia visiwani Zanzibar mapema wiki hii na kwa siku chache walikuwa wakipewa mbinu mbalimbali za kuwazuia Waarabu wasiweze kufurukuta kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza.
Kocha Hans Pluijm, anaijua vema Al Ahly kwani aliumana nao mwaka juzi na kutoka kuitungua bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya kwenda kupoteza Alexandria, Misri kwa mikwaju ya penalti hivyo amewakalisha chini wachezaji wake na kuwaambia watulize akili.
Habari za ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa, wachezaji Yanga wamekuwa wakielekezwa namna ya kuwazuia wachezaji wa Al Ahly kutoingia kwenye ‘boksi’ lao sambamba na kuwanyima fursa ya kumiliki mipira kwa muda mrefu.
“Wachezaji wa timu za Kaskazini hawafai kupewa nafasi ya kumiliki mipira wala kuingia kwenye 18 ya timu wenyeji, wana hila, hivyo vijana wamepewa mbinu za kuwakabia nje na kuepuka kufanya fauli zisizo za lazima,” chanzo kilisema.
“Pia safu ya ulinzi na viungo wamepewa jukumu la kuhakikisha Wamisri hawapumui wala kumiliki mpira muda mrefu, huku safu ya mbele wakiwa na jukumu la kumaliza kazi mapema ndani ya dakika 45 za kwanza,” kiliongeza chanzo hicho

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm hakupenda kuweka kila kitu wazi, lakini alisema amekuwa akikaa na wachezaji na kuwaambia kazi iliyo mbele yao na wajibu wao wa kujijengea heshima kwa mashabiki wao
Mdachi huyo ambaye ni swahiba na kocha wa Al Ahly, Martin Jol ambaye wanatoka nchi moja ya Uholanzi, alisema; “Tumefanya kazi ya kutosha na maandalizi yetu yako vizuri, wachezaji wana morali na imani yangu tuna kila sababu ya kushinda mchezo huu endapo watafanya kama tulivyojipanga na kesho (leo) asubuhi tunatajia kurudi Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho.”
“Hadi sasa mchezaji ambaye nitamkosa kwenye mechi ni Niyonzima kwa sababu ya kadi mbili za njano alizokuwa nazo, matatizo mengine kama majeruhi nitajua mara baada ya mazoezi ya mwisho kesho (leo) Ijumaa asubuhi,” alisema Pluijm.
“Tunacheza nyumbani, tunachotakiwa ni kujihamini, tucheze mpira wenye malengo na kushambulia kuhakikisha tunapata matokeo mazuri hapa nyumbani, tumeelekezana na tunaweza, kikubwa kilichobaki ni kukamilisha pale uwanjani,” aliongeza Pluijm.

Chanzo: Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment