Friday, December 15, 2017

IJUE HISTORIA YA WAPINZANI WA YANGA KLABU BINGWA AFRIKA 2018

Kati ya Februari 9 na 11, 2018 mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Yanga SC watawakaribisha wapinzani wao St. Louis kutoka nchini Ushelisheli katika mzunguko wa awali wa michuano ya klabu bingwa Afrika.


St. Louis ni mabingwa watetezi wa ligi ya Ushelisheli msimu wa 2016-17, ubingwa uliowapa tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika ikiwa imepita miaka 21 tangia wapata fursa ya kushiriki michuano hii mikubwa kabisa barani Afrika.

Timu hii toka visiwa vya Ushelisheli vyenye watu takribani 93,000 kwa sensa ya mwaka 2016, kuanzia mwaka 1979 ilipoanzishwa ilijulikana kama St. Louis FC kabla ya kubadilishwa jina mwaka 1994 na kuitwa Sun Shine SC.

Mwaka 2004 vikao ndani ya kanisa Katoliki nchini Ushelisheli viliazimia kulirudisha jina la zamani la St. Loius lakini kukawa na upinzani mkali kwa wale walioilea timu chini ya jina la Sun Shine SC.

Mwaka 2007 makubaliano yalifanyika na klabu hii kukubaliwa kutumia majina yote mawili. Yaani St. Louis Sun Shine United.

Ni timu ambayo ipo chini ya mwenyekiti mzee Jeff Cooper moja ya wafanyabiashara wakubwa nchini humo. Amekuwa akiijenga vyema timu hiyo ili kufikia malengo yake kwa usajili mzuri, malazi na masilahi ya wachezaji kwa kutafuta wadhamini kila pembe.

Ni timu inayotumia mfumo wa 4-4-2 na mara chache kubadilika kwa kuingia katika mfumo wa 4-3-3 na hii ni falsafa ya kocha wao Paul Khan aliyepata kusomea taaluma yake ya ukocha nchini Holland.

Ikitambulika kama St Louis kuanzia mwaka 1979 iliweza kunyakua vikombe 13 vya ligi na mara moja mwaka 1995 kama Sun shine SC. Na wamechukua mara moja (1) kama St. Louis Sun shine United . Hii inawafanya kuwa mabingwa wa muda wote katika ligi ya Ushelisheli kwa kubeba kombe la ligi mara 15 toka ligi hiyo ianzishwe mwaka 1979 sanjari na umri wa timu hiyo.

Michuano ya klabu bingwa Afrika wameshiriki mara tano na msimu huu wa 2018 itakuwa ni mara yao ya sita!. Katika mara tano zote walizoshiriki hawajawahi kuvuka raundi ya pili zaidi ya kutoka raundi ya kwanza tu.

Wachezaji wa kutumainiwa wa kikosi chao ni kiungo Mathiot Steve huvaa jezi namba 30 toka nchini Nigeria. Amechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa timu hii kutwaa ubingwa wa ligi yao msimu uliopita. Alitengeneza assits 13 na kufunga magoli 7 akicheza kama kiungo namba nane na mshambuliaji namba mbili.

Danilo Saljevic ndio kiungo wao mkabaji wenyewe humwita ' white dog ' . Huyu ana asili ya ufaransa akitokea visiwa vya Cape Verde.

Hao ndio St. Louis suns United watakaoikabili Yanga SC bingwa mara 27 wa ligi kuu Tanzania bara, bingwa mara 5 Kagame Cup wakiwa na rekodi ya kufika hatua ya makundi klabu bingwa Afrika mwaka 1998 na kombe la Shirikisho mwaka 2016.
CHANZO: Naipenda Yanga FB page.

0 comments:

Post a Comment