Sunday, March 19, 2017

Real Madrid yaitimulia vumbi Barcelona, yaitandika Athletic Bilbao 2- 1, tofauti ya point sasa ni 5 michezo sawa.



Timu ya Real Madrid jana jioni iliendelea kujihakikishia nafasi ya kutwaa kombe la ligi kuu ya Hispania ‘Spain - LaLiga Santander’ baada ya kuichapa timu ngumu ya Athletic Bilbao 2 – 1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Athletic Bilbao uitwao San Mames Barria.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute, uliwachukua Madrid dakika 25 kujipatia goli la kuongoza baada ya Karim Benzema kumalizia kazi ya mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo.

Athletic Bilbao wakicheza kwa kujiamini na kuuutawala zaidi mchezo karibu muda wote na kusababisha wachezaji wane wa Real Madrid kufanya madhambi na kuadhibiwa kwa kadi za njano kwa dakika tofauti dakika ya 28 Daniel Carvajal(RM) na Aritz Aduriz(AB) walivimbishiana kifua na refa kuwaadhibu wote kwa kadi za njano.

31’ Casemiro nae alipewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya, Toni Kroos na Keylor Navas dakika za 71 na 90 pia walionywa kwa kadi za njano.

Mpaka mapumziko Real Madrid walikuwa na goli moja wenyeji wakiwa 0.

Kipindi cha pili dakika ya 65 Raul Garcia alifanya kazi kubwa na kumuachia mpira Aritz Aduriz ambae na yeye aliitumia vizuri na kuandika goli kwa timu yake na kufanya ubao wa matangazo usomeke 1 – 1.

Kona iliyopigwa na Toni Kroosdakika ya 68 ilitua kwenye kichwa cha Cristiano Ronaldo ambae aliuparaza mpira huo na kumkuta Casemiro ambae aliukwamisha mpira huo wavuni na kuipatia Madrid goli la pili na la ushindi.

Kwa ushindi huo Madrid wamefikisha pointi 65 katika michezo 27 huku Barcelona wao wakiwa na pointi 60 kwa michezo 27.

Matokeo ya michezo mingine ya jana march 18 ni kama ifuatavyo.
Real Betis 2 - 0 Osasuna
Eibar 1 - 1 Espanyol

Alaves 1 - 0 Real Sociedad


Michezo mitano kupigwa leo jumapili

Leganes VS Malaga  14:00
Atletico Madrid VS Sevilla  18:15
Sporting Gijon VS Granada 20:30
Deportivo La Coruna VS Celta Vigo 20:30

Barcelona VS Valencia  22:45
Msimamo wa Spain - LaLiga Santander baada ya jana march 18

0 comments:

Post a Comment