Sunday, February 12, 2017

Yanga Yafanya Mauaji Comoro

Klabu ya Young Africans maarufu kama Yanga, leo ilishuka dimbani huko visiwani Comoro kukipiga na Ngaya CM katika mchezo wa kwanza wa klabu bingwa barani Africa (CAF Champions 2016/17).

Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa magoli 5-1 dhidi ya wenyeji Ngaya, matokeo ambayo yanaiweka Yanga katika nafasi kubwa ya kuweza kusonga mbele katika raundi inayofuata mara baada ya mechi ya marudiano itakayopigwa jijini Dar, majuma kadhaa yajayo.

Karamu hiyo ya magoli kwa upande wa Yanga yalipachikwa kimiani na Justin Zullu 43', Saimon Msuva 45', Obrey Chirwa 59', Tambwe 65'  huku Thaban Kamusoko akihitimisha kipigo hicho kwa kupachika goli la 5 mnamo dakika ya 73'.

Dakika ya 66' Ngaya walifanikiwa kujipatia goli la kufutia machozi lililotupiwa kimiani na mchezaji Anfane.

Hadi dakika 90 zinamalizika Yanga SC 5-1 Ngaya CM.

0 comments:

Post a Comment