Thursday, February 16, 2017

Bayern Munich 5 - 1 Arsenal, Real Madrid yafanya mauaji ligi ya mabingwa ulaya



Huko katika dimba la Allianz Arena wenyeji  Bayern Munich wameifanyia kitu kibaya Arsenal ya Uingereza baada ya kuitandika bila huruma 5 – 1.

Mchezo ulianza kwa kushambuliana huku kila timu ikilenga kupata goli la mapema, lakini bahati iliwaangukia wemyeji Bayern mnamo dakika ya 11 pale Arjen Robben alipomchungulia golikipa wa Arsenal David Ospina ambae alitoka golini na kuandika goli la kwanza.

Arsenal  walipata penati 30’ baada ya Robert Lewandowski kumfanyia madhambi Laurent Koscielny katika eneo la hatari na mwamuzi  Milorad Mazic kutoka Serbia aliamuru upigwe mkwaju wa penati.
Penati ilipigwa na Alexis Sanchez 30’ lakini uhodari wa kipa Manuel Neuer alipangua penati hiyo kabla ya kumkuta tena Alexis Sanchez aliemalizia na kuisawazishia arsenal.

Hadi mapumziko Bayern Munich 1 – 1 Arsenal.

Kipindi cha pili dakika ya 53 Robert Lewandowski alipachika goli la pili kwa kichwa baada ya majaro safi toka wingi ya kulia.

Akiwa yeye na goli kipa Thiago Alcantara aliweza kuipatia Bayern Munich goli la tatu, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Robert Lewandowski 56’.

Dakika 63 Thiago Alcantara alifunga goli la nne baada ya Francis Coquelin kukosea kuokoa mpira  na kumkuta mfungaji ambae alitumia akili za ziada kuukwamisha mpira wavuni.


Goli la mwisho liliwekwa kimiani na Thomas Mueller dakika 88’.


Vikosi vilikuwa:

Bayern Munich:   Manuel Neuer, Philipp Lahm, David Alaba, Mats Hummels, Javier Martinez, Xabi Alonso, Arturo Vidal, Arjen Robben, Douglas Costa 84’,  Thiago Alcantara, Robert Lewandowski 86’.

Sub: Joshua Kimmich 84’, Thomas Mueller 86’, Rafinha 88’, Juan Bernat, Sven Ulreich, Kingsley Coman, Renato Sanches.

Kcha: Carlo Ancelotti

Arsenal:
David Ospina, Hector Bellerin, Kieran Gibbs, Shkodran Mustafi, Laurent Koscielny 49’, Francis Coquelin 77’, Granit Xhaka, Alex Iwobi 66’, Alex Oxlade-Chamberlain, Mesut Oezil, Alexis Sanchez.
Sub:
Gabriel Paulista 49’, Theo Walcott 66’ Olivier Giroud 77’, Nacho Monreal, Danny Welbeck, Petr Cech, Mohamed Elneny.
Kocha: Arsene Wenger.

Huko Estadio Santiago Bernabeu
FT
Real Madrid 3 – 1 SSC Napoli

Real Madrid: Karim Benzema 19’, Toni Kroos 49’ na Casemiro 54’.



SSC Napoli:   Lorenzo Insigne 8’ 



0 comments:

Post a Comment