Serikali yatoa katazo juu ya simba na yanga kuuutumia uwanja wa taifa na kuwaambia watafute pakuchezea mechi zao. Hayo yamesemwa na waziri anaehusika na michezo mheshimiwa Nape.Nape alisema hivi
“Uwanja huu sasa hautatumika na Yanga na Simba, hawawezi kufanya uharibifu huu wa makusudi huku wakijua kwamba uwanja huu ndani yake kuna kodi za walipa kodi,Mmeona walichofanya na sasa wanaweza kutafuta sehemu ya kwenda kucheza, watafute uwanja wa kutumia, hadi hapo tutakapoamua vinginevyo,Wanaotakiwa kuutumia ni ukiwa mzuri na si kama ulivyo sasa, wako wengine wastaarabu wanaweza kuutumia."
Hii inatokana na mashabiki wa kilabu ya simba kuvunja viti na kufanya fujo kubwa iliyozua taharuki kubwa kwa kile walichookiita kuonewa waziwazi na waamuzi wa mchezo wa jana.
0 comments:
Post a Comment