Sunday, September 11, 2016

MOURINHO AWATAJA WALIOICHOMESHA UNITED DHIDI YA MAN CITY

Kocha asiyeisha Mbwembwe, maneno mengi na visingizio lukuki pale anapofanya vibaya, Jose Mourinho, kwa mara nyingine tena ameibuka na kuwanyooshea vidole baadhi ya wachezaji katika kikosi chake kilichocheza jana na Man City kuwa ndio wamesabibisha kipigo hicho katika dimba lao la nyumbani.

Kama ilivyo kawaida yake Mourinho amewanyooshe vidole wachezaji, Mkhitaryan, Lingard, Blind pamoja na Baily kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Mourinho aliwaambia wachezaji hao kipindi cha mapumziko kuwa walikuwa wanavurunda uwanjani ila tu busara zake ndo zilifanya wachezaji hao waendelee kubaki uwanjani bila kuwatoa.

"Tulikuwa na tatizo la kiwango kibovu" alisema Mourinho.

"Tulikuwa tunapoteza mipira kirahisi sana,hata walinzi wetu wa kati ambao walikuwa katika kiwango cha juu kipindi cha nyuma ila leo wamepoteza mipira kirahisi sana"

Yalikuwa maneno ya Mourinho baada ya kushuhudia vijana wake wakipokea kichapo cha mabao mawili kwa moja katika uwanja wao wa nyumbani hapo jana.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

Related Posts:

  • CLAUDIO RANIERI AIONYA MAN UNITEDClaudio RanieriKocha Wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza Leicester City, Claudio Ranieri ameionya Man United kuwa wasitegemee mchezo rahisi leo. Ranieri amedai anaamini kuna kitu kizuri kinakuja katika klabu yak… Read More
  • MAISHA YA FABREGAS CHELSEA YAFIKA UKINGONI Cesc Fabregas ameambiwa na kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte kuwa anaweza kuondoka klabuni hapo. Conte ametoa kauli hiyo huku kukiwa kumebaki siku 2 tu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya. Kiungo h… Read More
  • DAVID MOYES AWANASA WAWILI KUTOKA MANCHESTER UNITED Boss Mpya wa klabu ya Sunderland, David Moyes amekamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka katika klabu ya Manchester United. Klabu ya Manchester United imethibitisha kuuzwa kwa wachezaji wao wawili ambao ni Paddy McNa… Read More
  • WEST BROM YAVUNJA REKODI YA KLABU USAJILI WA CHADLI Klabu ya West Bromwich Albion imevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumsajili Winga wa Tottenham Spurs kwa kitita cha Pauni milioni 13. Chadli alijiunga na Spurs akitokea FC Twente kwa uhamisho wa pauni milioni 7 Julai 2013… Read More
  • NYOTA WA ZAMANI WA MAN UNITED AITABIRA UBINGWA CHELSEA Paul Scholes anasema Chelsea wana nafasi ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu Nchini Uingereza. Chelsea inaongoza ligi hiyo kufuatia ushindi mnono katika mechi zake tatu ambazo imekwishacheza hadi hivi sasa chini ya kocha Mpya… Read More

0 comments:

Post a Comment