Kocha Wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza Leicester City, Claudio Ranieri ameionya Man United kuwa wasitegemee mchezo rahisi leo.
Ranieri amedai anaamini kuna kitu kizuri kinakuja katika klabu yake kuelekea mchezo wao leo dhidi ya Mashetani wekundu nchini ya kocha Mourinho mchezo wa ngao ya Jamii.
"Nafanya kazi katika ari ileile, kujiamini kulekule na mtazamo uleule" alisema Ranieri.
"Hakuna kilichopungua, ni jukumu langu kuhakikisha wachezaji wangu wanakuwa na njaa ileile ya mafanikio" Aliongeza Mreno huyo aliyeipa ubingwa wa kihistoria Leicester.
Ranieri bado anaendelea kuwa na imani kubwa na kikosi chake na anajua wazi kuwa anapaswa Leicester kucheza katika ari ileile iliyopelekea kutwaa ubingwa wa EPL msimu wa 2015/16.
"Uimara wetu si katika kumiliki mpira, ni kucheza vile tunavyotaka cha msingi ni kuwa fiti asilimia 100, hivyo haitakuwa kazi rahisi kwa Manchester United leo ndani ya dakika 90".
0 comments:
Post a Comment