Boss Mpya wa klabu ya Sunderland, David Moyes amekamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka katika klabu ya Manchester United.
Klabu ya Manchester United imethibitisha kuuzwa kwa wachezaji wao wawili ambao ni Paddy McNair na Donald Love waliojiunga na klabu ya Sunderland kwa jumla ya ada ya uhamisho ya pauni 5.5 kwa wachezaji wote wawili.
Wawili hao wameenda kuungana na kocha wao wa zamani David Moyes na tayari usajili huo umeshakamilika na kuthibitishwa na klabu zote mbili.
McNair 21, alijiunga na Manchester United mwaka 2011 baada ya kuonwa na mascouti wa klabu hiyo lakini hakuwahi kucheza hadi Van Gaal alipoichukua timu na kwa mara ya kwanza akaichezea United katika msimu huo.
Akizungumzia usajili huyo Moyes amesema analengo la kuongeza wachezaji makinda kwenye kikosi chake pamoja na wakongwe ili kwa umoja wao waweze kuleta matunda katika kikosi hicho.
"Nataka kuongeza wachezaji makinda kwenye kikosi pamoja na wakongwe. Nataka niwalete wachezaji ambao watakuwepo hapa (klabuni) kwa muda mrefu na muda mfupi na natumai hawa wawili watakuwepo kikosini kwa muda mrefu"

0 comments:
Post a Comment