Thursday, August 11, 2016

RASMI:LIVERPOOL WAMNASA NYOTA WA ZAMANI WA MADRID

Moja kati ya usajili wa kushangaza kabisa katika kipindi hiki cha Usajili.

Jonathan 36, kwa sasa ameshastaafu kucheza soka, Jonathan Woodgate aliachana na Middlesbrough Mwezi May mwaka huu baada ya mkataba wake kumalizika.

Wakati akicheza soka, Woodgate aliwahi kuzitumikia klabu za Leeds, Newcastle, Real Madrid, Tottenham pamoja na Stoke City.
Pia amekuwa Nahodha wa timu yake ya taifa ya Uingereza kwa vipindi vinane.

Licha ya kuachana na maisha ya soka na kuamua kupumzika na familia yake, Woodgate amekubali kusaini mkataba Liverpool akiwa kama Scout wa timu hiyo na kwamba ataelekeza nguvu zake katika nchi za Hispania na Ureno.

0 comments:

Post a Comment