Sunday, June 12, 2016

YANGA YATUMA MAJINA YA NYOTA WAO WAPYA CAF

Klabu ya Yanga imewasilisha majina ya wachezaji wake CAF waliowasajili hivi karibuni ambao ni Hassan Ramadhan Kessy, Juma Mahadhi, Vicent Andrew na Beno Kakolanya kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo katika kombe la shirikisho Afrika CAF.

Hans amesema ameridhika na viwango vya wachezaji hao kutokana na kile walichokionyesha kwenye mazoezi ya timu.

"Nimeridhika kabisa na uwezo waliouonyesha kwenye mazoezi ya siku mbili tatu ndiyo maana tukayatuma majina yao nikiamini watakuwa na msaada kwetu hasa kutokana wamekuja kwenye timu ya ushindi" alisema Pluijm.

Yanga sasa imebakisha nafasi mbili ili kujaza kikosi chao baada ya kuwanasa hao wanne.
Mechi ya kwanza ya hatua hiyo ya makundi Yanga itacheza na MO Bejaia ya nchini Algeria, mchezo utakaopigwa huko nchini Algeria tarehe 19, Juni, 2016.

0 comments:

Post a Comment