Saturday, June 11, 2016

SIMBA YAMNASA WINGA MACHACHARI, ASAINI MIAKA 2

Klabu ya Simba Sports Club imefanikiwa kumsajili mchezaji wa Mwadui FC, Jamali Mnyate aliyesaini mkataba wa miaka 2 kwa uhamisho wa Tsh. Milioni 15.



Kufuatia usajili huo Makamu Rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange Kaburu amesema, kwa muda mrefu walikuwa wanamfukuzia mchezaji huyo na sasa wanafurahi sana kujiunga na klabu yao.

Kaburu amesema tayari wamemalizana na mchezaji huyo na sasa ni mchezaji halali wa Simba.

"Baada ya kuondoka Ramadhani Singano tulimkossa mtu mwenye kasi na msimu uliopita tumepata sana tabu ndiyo maana tukakubaliana kumsajili Mnyate ambaye kwa kiwango alichonacho tunaamini atatusaidia katika mipango yetu ya kurudi kwenye ubora wetu msimu ujao" alisema Kaburu

0 comments:

Post a Comment